Dini ya Uislamu

Inatangazwa kupitia Dalili zitokanazo na Qur'ani na Sunnah za Mbora wa Viumbe.

Mafundisho ya Uislamu na Tabia zake

A- Maamrisho.

Hizi ni Baadhi ya Tabia za uislamu na Adabu zake ambazo zinapupia juu ya kuifunza tabia njema jamii ya kiislamu, na tutazitaja kwa ufupi kwa kuzingatia uchambuzi wa tabia hizi, na tabia hizi zinatokana na misingi mikuu ya uislamu, ambayo ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu( Qur’ani tukufu) na Hadithi za Bwana Mtume -Rehema za mwenyezi mungu ziwe juu yake na Amani –

Kwanza: Ukweli katika mazungumzo:

Uislamu unawalazimisha wafuasi wake wenye kujinasibisha kwake kuwa wakweli wakati wa mazungumzo, na unawawekea kuwa ni alama ya kudumu nayo ambayo haifai kwa hali yoyote kuepukana nayo, na unawatahadharisha kwa tahadhari kubwa juu ya uongo, na unawakataza kwa ibara za hali ya juu sana kwa kuwakataza, na kwa sifa iliyowazi ya katazo hilo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkaitumia sheria Yake! Fuateni maamrisho ya Mwenyezi Mungu na epukeni makatazo Yake katika kila kitu mnachokitenda na mnachokiacha, na kuweni pamoja na wakweli katika Imani zao na ahadi zao na katika kila jambo miongoni mwa mambo yao.

[Surat Taubah 119]

Na Amesema Mtume wa Allah rehema na amani za Allah ziwe juu yake:

Kutoka kwa Abdillah bin Mas’udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema za mwenyezi mungu ziwe juu yake na Amani -: “Shikamaneni na ukweli, kwani ukweli hupelekea katika wema, na hakika wema hupelekea katika pepo, na hatoacha mtu kuwa mkweli na akishughulika na ukweli mpaka ataandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni mkweli, na tahadharini na uongo, kwani uongo unapelekea katika uovu, na hakika uovu hupelekea katika moto, na hatoacha mtu kuendelea kuwa muongo, na akishughulika na uongo mpaka ataandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni muongo”.

Ameitoa Bukhariy (6094) na Muslim 2607

Na uongo si katika sifa za waumini bali ni sifa za wanafiki [7] Amesema Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-:

“Alama za Mnafiki ni tatu: Anapozungumza husema uongo, na anapoahidi huenda kinyume, na akiaminiwa hufanya hiyana”.

[7] Mnafiki ni yule mtu ambaye anajidhihirisha kuwa ni muislamu lakini kiuhalisia itikadi yake moyoni haiamini dini ya uislamu.

[8] Hadithi amaeitoa Bukhariy katika kitabu cha Imani ,Mlango wa alama za wanafiki(1/15)

Hivyo wanasifika maswahaba watukufu na sifa za ukweli mpaka akasema mmoja wao: hatukuwa tukiujua uongo katika zama za Mtume -Rehema za mwenyezi mungu ziwe juu yake na Amani.

Ya pili: Kutekeleza amana na kutimiza makubaliano na mikataba, na kufanya uadilifu kwa watu.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzifikishe amana kwa watu wake na pindi mnapo wahukumu watu basi muwahukumu kwa uadilifu}

[An Nisaai: 58].

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Na tekelezeni Ahadi Kwa hakika ahadi ni yenye kuulizwa}

“Na timizeni kipimo wala msikipunguze mnapowapimia wasiokuwa nyinyi, na mfanye mizani ya sawa, kwani kufanya uadilifu katika upimaji wa vibaba na mizani ni bora kwenu nyinyi ulimwenguni na kuna mwisho mwema mbele ya Mwenyezi Mungu kesho Akhera”.

[Surat Israa 34-35]

Na akawasifu waumini kwa kauli yake.

“Wale wanaotekeleza ahadi ya Mwenyezi Mungu Ambayo Aliwaamrisha kwayo na hawaitengui ahadi ya mkazo ambayo walimuahidi nayo Mwenyezi Mungu”.

[Ar Ra’di: 20].

Ya tatu: Unyenyekevu na kutokuwa na Kiburi.

Na kwa hakika alikuwa Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- ni mnyenyekevu mno kuliko watu wengine, akikaa na maswahaba wake anakuwa kama mmoja wao, alikuwa hapendi kusimamiwa na watu anapofika mahala na kwa hakika ilikuwa akijiwa na mtu mwenye Haja humshika mkono na kuondoka naye na hamrudishi mpaka amtimizie haja zake, na kwa hakika aliwaamrisha waislamu kuwa ni wanyenyekevu na akasema: (Hakika Mwenyezi Mungu alinifunulia wahyi kuwa tunyenyekeane mpaka asiweze kujifaharisha mmoja kwa mwingine, wala asimfanyie yeyote uadui mwingine)

(9) Hadithi ameitoa Bukhari na Muslim(17/200) Kitabu cha mlango wa sifa ambazo hujilikanwa nazo watu wa peponi.

Ya Nne: Ukarimu na utoaji katika njia za kheri.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na mali yoyote mnayoitoa, nafuu yake itawarudia nyinyi wenyewe kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na Waumini hawatoi isipokuwa kwa kutafuta radhi ya Mwenyezi Mungu. Na mali yoyote mnayoitoa, kwa kumtakasia Mwenyezi Mungu, mtapewa kikamilifu thawabu zake na hamtapunguziwa chochote katika hizo. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya Uso kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakata na kila sifa pungufu (waj-hu Allah) kwa namna inayonasibiana na Yeye.

[Baqarat 272]

Na kwa hakika amewasifu Mwenyezi Mungu Waumini kwa kauli yake:

“Na wanalisha chakula, pamoja na kuwa wanakipenda na kukihitajia, kumpa fukara asiyeweza kuchuma, asiyemiliki chochote katika vitu vya kiulimwengu, na kumpa mtu aliyetekwa vitani miongoni mwa washirikina na wengineo”,

[Al- insaan 8]

Ukarimu na moyo mzuri ni sifa za Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na ni sifa za waumini wenye kumfuata, hakubakii kwake chochote katika mali isipokuwa hukitoa katika njia ya kheri. Amesema Jabir radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu-ni mmoja kati ya maswahaba wa Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-

“Hakuwahi kuombwa Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani – kitu chochote akasema hapana”.

Na amehimiza juu ya kumkirimu mgeni na akasema:

“Yeyote mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi asimuudhi jirani yake, Na Yeyote mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na amkirimu mgeni wake, Na Yeyote mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na aseme la kheri au anyamaze.”

(10) Ameitoa Bukhari (6138),na Muslim(47)

Ya Tano: Subira na kuvumilia matatizo:

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Na subiri kwa yote yatakayo kupata hakika hayo ni katika mambo yanayostahiki kuazimiwa (na kila mtu)

[Luqman 17]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Enyi Mlioamini, takeni msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yenu yote, kwa kusubiri juu ya mikasa na misiba, na kuacha maasia na madhambi na kusubiri juu ya kufanya mambo ya utiifu na yale yanayomkurubisha mtu kwa Mola wake, na kwa Swala ambayo kwayo nafsi inapata utulivu na ambayo inakataza machafu na maovu. Hakika Mwenyezi Mungu Yuko pamoja na wenye kusubiri”.

[Al-baqara 153]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Na hakika tutawalipa wale waliosubiri malipo yao kwa mazuri zaidi kuliko yale waliyokuwa wakiyafanya}

[An-nahli 96]

Na kwa hakika Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- alikuwa ni miongoni mwa watu wenye subira ya hali ya juu, na pia mvumilivu katika maudhi na alikuwa halipizi ubaya kwa ubaya, watu wake walimuudhi naye akiwalingania kuingia katika uislamu na walimpiga mpaka wakamtoa damu usoni kwake akawa anafuta damu usoni huku akisema:

“Ewe Mola wangu wa haki wasamehe watu wangu kwani kwa hakika hawajui walifanyalo” [11]

[11] Hadithi ameitoa Bukhariy katika kitabu cha wenye kuritadi mlango(5) (9/20)

Ya Sita: Haya (Aibu):

Muislamu halisi hujizuia na machafu na huwa mwenye haya, na haya ni sehemu katika imani, na haya humsukuma mtu katika kila tabia njema, na inamzuia kuwa na kauli chafu na kufanya machafu yawe maneno au matendo, Na amesema Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-:

“Haya (Aibu) haiji ila kwa kheri”

[12] Hadithi ameitoa Bukhariy katika kitabu cha Adabu mlango wa Haya (8/35)

Ya Saba: Kuwatendea Wema wazazi wawili:

Kuwatendea wema wazazi wawili na kuamiliana nao vizuri na kujishusha kwa ajili yao ni katika wajibu wa msingi katika dini ya uislamu, na uwajibu huu huzidishiwa mkazo zaidi kila wanavyozidi wazazi wawili kuzeeka na kuwahitaji wazazi wawili, na kwa hakika ameamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwafanyia wema katika Kitabu chake kitukufu na akatilia mkazo utukufu wa haki zao na akasema Mwenyezi Mungu – kutakasika na machafu ni kwake:

{Na amehukumu Mola wako yakuwa msimuabudu isipokuwa yeye na wazazi wawili kuwatendea wema, na ikiwa mmoja wao atafikia uzee naye yu pamoja nawe au wote wawili basi usiwaambie hata ‘Aah!’ wala usiwakemee, na sema nao maneno yaliyokuwa mazuri}

Na uwe, kwa mama yako na baba yako, mdhalilifu na mnyenyekevu kwa kuwahurumia, na umuombe Mola wako awarehemu kwa rehema Zake kunjufu wakiwa hai na wakiwa wamekufa, kama walivyovumilia juu ya kukulea ulipokuwa mdogo usiokuwa na uwezo wala nguvu”.

[Al-israa].

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na tumemuusia mwanadamu kuwatendea wema wazazi wake wawili na kuwafanyia hisani, Mama yake alimbeba tumboni, shida juu ya shida, na mimba yake na kumaliza kunyonya kwake ni ndani ya kipindi cha miaka miwili, na tukamwambia, «Mshukuru Mwenyezi Mungu kisha uwashukuru wazazi wako, kwangu mimi ndio marejeo nipate kumlipa kila mmoja kwa anachostahili”.

[Luqman: 14].

Na alimuuliza mtu mmoja Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- (Ni nani ambaye ana haki zaidi ya kuishi naye vizuri) Akasema:

(“Mama yako”, akasema, kisha nani, akasema: “Mama yako” ,akasema kisha nani, akasema: “Mama yako,” akasema: kisha nani? akasema “Baba yako” [13]

(13) Hadithi hii ameitoa Bukhariy katika Kitabu cha adabu mlango wa nani mwenye haki zaidi wakuamiliana nae vizuri(8/2)

Na kwa hivyo basi uislamu unamlazimisha muislamu kuwatii wazazi wake wawili katika kila wanalomuamrisha kulifanya isipokuwa itakapokuwa ni katika kumuasi Mwenyezi Mungu wakati huo hairuhusiwi kumtii kiumbe katika kumuasi Mwenyezi Mungu, Amesema Mwenyezi Mtukufu:

{Na ikiwa wazazi wako watakushurutisha kunishirikisha mimi kwa jambo ambalo huna ujuzi nalo basi usiwatii lakini kaa nao hapa duniani kwa wema}

[Luqman: 15].

Kama ambavyo ni wajibu kuwafanyia upole na kujishusha kwa ajili yao na kuwakirimu kwa maneno na vitendo na kuwafanyia wema wa kila aina kwa kadiri ya uwezo wake kama kuwalisha na kuwavisha na kuwatibu maradhi yao na kuwakinga na mabaya na kuwaombea dua na kuwatakia msamaha na kutekeleza ahadi zao na kuwakirimu marafiki zao.

Ya Nane: Kuamiliana kwa Tabia njema na watu wengine:

Amesema Mtume rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani:

(Muumini aliyekamilika kiimani zaidi ni yule mwenye tabia njema zaidi kuliko wengine)(14)

(14) Hadithi ameitoa Abuu Daudi katika kitabu cha Sunnah mlango wa kuzidi imani na kupungua(5/6),na Tirmidhiy katika kitabu cha unyonyeshaji mlango ulikujakuelezea haki za mwanamke kwa mume wake (3/457)na kasema Tirmidhiy: hadithi hii ni nzuri na sahihi amesema albaniy: angalia sahihi ya Abii Daudi(3/886)

Amesema Mtume Rehema za mwenyezi mungu ziwe juu yake na amani:

(Hakika miongoni mwa wenye kupendeza zaidi kwangu mimi na watakao kaa karibu yangu zaidi siku ya kiyama ni wale wazuri wenu wa tabia) (15)

{15} Hadithi ameitoa Bukhariy: Kitabul manaaqib ,mlango,wa sifa za mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani(4/230) kwa tamko (Hakika katika wabora wenu ni wale wazuri wenu wa tabia)

Na akamsifia Mtume wake -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- kwa kauli yake:

“Na hakika wewe, ewe Mtume, ni mwenye tabia njema”.

[Al Qalam: 4].

Na Amesema Mtume Rehema za mwenyezi mungu ziwe juu yake na na amani:

“Kwa hakika nilitumwa ili kukamilisha tabia njema”(16)

Kwa hivyo yapasa kwa muislamu kuwa na tabia njema kwa wazazi wake hali ya kuwafanyia wema kama tulivyokwisha sema, kuwa na tabia nzuri kwa watoto kwa kuwalea malezi mema na kuwafundisha uislamu na kuwaweka mbali na kila linalowadhuru hapa Duniani na akhera, awape matumizi kutoka katika mali yake mpaka watakapofikia umri wa kuweza kujitegemea wenyewe na kuwa na uwezo wa kujitafutia.

na vile vile anatakiwa awe na tabia njema kwa mke wake na ndugu zake na dada zake na ndugu zake wa karibu na majirani zake na watu wote, awapendelee ndugu zake kama anavyojipendelea yeye nafsi yake na awe ni mwenyekuunga udugu na majirani zake ,na awaheshimu wakubwa wao na kuwaonea huruma wadogo zao na awatembelee na kuwaliwaza waliopata matatizo kwa kuifanyia kazi kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na wafanyieni Ihsani (wema) wazazi wawili na jamaa na Mayatima na Masikini na Majirani na jirani walio karibu na majirani walio mbali na marafiki walio ubavuni na msafiri aliyeharibikiwa”.

[An Nisaai: 36].

Na kauli ya Mtume Rehema za mwenyezi mungu ziwe juu yake na amani:

(Yeyote mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na asimuudhi jirani yake)(17)

(16) Hadithi ameitoa Imamu Ahmad katika (17/80) na amesema Ahmad Shaakir kuwa isnad yake ni sahihi,na ameitoa Bukhariy fil adabu ,na Baihaqiy katika mlango wa imani na Haakim katika Mustadrak.

(17) Hadithi ameitoa Bukhariy katika mlango wa Adabu,mlango wa mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na asimuudhi jirani (8/13).

Ya Tisa: Kupigana Jihadi Katika Njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ili kumnusuru aliyedhulumiwa na kuisadikisha haki na kusambaza uadilifu.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na piganeni, enyi Waumini, ili kuinusuru dini ya Mwenyezi Mungu, na wale wanaopigana nanyi, wala msifanye yaliyokatazwa ya kukatakata viungo, kufanya hiyana (ya kuchukua kitu katika ngawira kabla ya kugawanywa), kumuua asiyefaa kuuawa miongoni mwa wanawake, watoto, wazee na wanaoingia kwenye hukumu yao. Hakika Mwenyezi Mungu Hawapendi wale wanaokiuka mipaka Yake na kuyahalalisha yalioharamishwa na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake”.

[Al-baqara 190]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na ni lipi linalowazuia, enyi Waumini, kupigana jihadi katika njia ya kuitetea dini ya Mwenyezi Mungu na kuwatetea waja Wake wanaodhalilishwa, miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto waliodhulumiwa, na ambao hawana ujanja wala njia ya kufanya isipokuwa ni kumtaka Mola wao Awanusuru wakimuomba kwa kusema, «Mola wetu, tutoe kwenye mji huu (Makkah) ambao watu wake wamejidhulumu nafsi zao kwa kukufuru na wamewadhulumu Waumini kwa kuwakera, na utuletee kutoka Kwako msimamizi wa kusimamia mambo yetu na mtetezi wa kututetea dhidi ya madhalimu»?

[An-saai75]

Lengo la jihadi katika uislamu ni kuithibitisha haki, na kueneza uadilifu kwa watu na kuwapiga vita wale wote wenye kuwadhulumu waja na wanawafukuza na kuwazuia kufanya ibada ya Mwenyezi Mungu na pia kuwazuia wasiingie katika uislamu, na Jihadi kwa upande mwingine inakataza fikira za kuwalazimisha watu kwa nguvu kuingia katika dini ya uislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Hakuna kulazimishwa katika dini}

[Albaqarat 256]

Na wakati wa vita haifai kwa muislamu kumuua mwanamke wala mtoto mdogo wala mzee aliyezeeka bali huuliwa Madhalimu wenye kupigana.

Na yeyote atakaye uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu basi mtu huyo ni shahidi na ana cheo na malipo na thawabu kwa Mwenyezi Mungu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Wala usidhani, ewe Mtume, kwamba wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu hawahisi chochote. Bali wao wako hai uhai wa barzakh (Akhera) kwenye ujirani wa Mola wao Ambaye walipigana jihadi kwa ajili Yake na wakafa katika njia Yake, inawapitia riziki yao huko Peponi na wananeemeshwa”.

{Wanafurahia aliyowapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila zake na wanawashangilia walioko nyuma yao ya kwamba haitokuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika}

[Al-Imran: 169،170].

Ya Kumi: Kuomba Dua Na kumtaja Mwenyezi Mungu na kusoma Qur’ani:

Kila inavyozidi Imani ya Muumini ndivyo unavyozidi mshikamano wake na Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumuomba yeye na kunyenyekea mbele yake katika kumkidhia haja zake hapa duniani na kumsamehe madhambi yake na makosa yake na kumuinua daraja siku ya mwisho, na Mwenyezi Mungu ni mkarimu anapenda kuombwa na waombaji. Amesema – kutakata na machafu ni kwake-

{Na ikiwa watakuuliza waja wangu kuhusu mimi, basi mimi niko karibu na jibu maombi ya mwenye kuniomba pindi atakaponiomba}

[Al Baqarah: 186].

Hivyo Mwenyezi Mungu anajibu dua atakapo kuwa mja ameomba kheri, na humlipa mja thawabu kwa maombi haya.

Na hivyo katika sifa za waumini ni kukithirisha kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu usiku na mchana kwa siri na kwa wazi basi na amtukuze Mwenyezi Mungu kwa kila aina ya kutukuza na kumtaja kwa mfano kusema: Sub-hanallah, Alhamdulillah, Walaa ilaaha illa llah, Wallahu Ak-baru, na dhikri nyingine katika matamshi ya kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa hakika amezipangia hizo dhikri ujira mkubwa na thawabu nyingi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu: Amesema Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-

(Wametangulia wapweke, wakasema maswahaba ni kina nani hao wapweke ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Akasema: “Ni wale wenye kumtaja Mwenyezi Mungu sana wake kwa waume)

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kwa vitendo, mtajeni Mwenyezi Mungu kwa nyoyo zenu, ndimi zenu na viungo vyenu utajo mwingi sana”.

{Na mumtakase asubuhi na jioni} Ahzaab: 41,42 na Amesema- kutakasika na machafu nikwake- {Basi nikumbukeni kwa kunitaja nami nitawakumbuka na mnishukuru mimi na wala msinikufuru}

[Al-baqra 152]

Na miongoni mwa Dhikri ni kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu – Qurani tukufu- kila anavyozidisha mja kusoma Qur’ani na kuizingatia cheo chake kinazidi kuwa juu kwa Mwenyezi Mungu.

[18] Hadithi ameitoa Muslim : kitabu cha Dhikri na Dua- mlango wa kuhimiza Dhikri (17/4)

Ataambiwa msomaji wa Qur’an tukufu siku ya kiyama:

{Soma na upande kama ulivyokuwa ukisoma ulimwenguni kwa upandishwaji wako daraja utaishia mwisho wa aya ambayo utakayoisoma) (19)

(19) Ameitoa Abuu Daud (1464) na tamko ni lake,na Tirmidhiiy (2914).An-nasai katika (sunanul kubraa)( 8056) na Ahmad(6799 )

Ya Kumi na moja: Kujifunza elimu ya kisheria na kuwafundisha watu na kuwalingania kutafuta elimu.

Amesema Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake:

“Yeyote atakaye fuata njia kwa nia ya kutafuta elimu, Allah humfanyia wepesi mtu huyo njia ya kwenda peponi, na kwa hakika Malaika wanawainamishia mbawa zao kwa kuridhia kwa anachokifanya- kutafuta elimu-(20)

[200] hadithi ameitoa Tirmidhiy Mlango wa elimu mlango wa fadhila za ibada(4/153),na Abuu Daud: kitabu cha elimu mlango wa kuhimiza juu ya kutafuta elimu(45857),na ibnu maajah katika muqaddimat (1/81)na ameisahihisha Albaniy(swahihul jaamiy(5/302)

Amesema Mtume Rehema za mwenyezi mungu ziwe juu yake na amani:

“Mbora wenu ni yule aliyejifunza Qur’ani na akaifundisha”

Amesema Mtume rehema za mwenyezi mungu ziwe juu yake na amani:

“Hakika Malaika wanamswalia mwenye kuwafundisha watu kheri” (22)

Amesema Mtume rehema za mwenyezi mungu ziwe juu yake na amani:

“Mwenye kulingania katika uongofu atapata malipo mfano wa malipo ya mwenye kuufanyia kazi na uongofu na haipunguzi katika ujira wake kitu chochote (23)

(21) Hadithi ameitoa Bukhariy katika kitabu cha fadhila ,Mlango wa mbora wenu ni yule mwenye kujifunza Qur’an na akifundisha (6/236)

(22) hadithi ameitoa Tirmidhiy katika kitabu cha elimu,mlango wa uliokuja kuzungumzia fadhila ufahamu wa ibada(5/50kwa matamshi marefu.)

(23) Ameitoa muslim katika kitabu cha elimu mlango mwenye kufufua sunnah nzuri au mbaya(227/16)

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Hakuna yeyote aliye na kauli nzuri zaidi kuliko yule anayelingania kupwekeshwa Mwenyezi Mungu na kuabudiwa Yeye Peke Yake, na anayesema, «Mimi ni katika Waislamu wanaofuata amri Ya Mwenyezi Mungu na Sheria Yake.» Katika aya hii kuna kusisitiza kulingania kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kueleza utukufu wa wanavyuoni wenye kulingania Kwake kwa ujuzi, kulingana na yale yaliyokuja kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani zimshukie.

[Fuswilat 33]

Ya kumi na mbili: Kuridhia Hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake:

Kutopinga jambo ambalo Mwenyezi Mungu amelifanya kuwa ni sheria, kwani Mwenyezi Mungu -kutakasika na machafu ni kwake- ndiye hakimu wa mahakimu wote, na ni mwenye huruma kuliko yeyote hakifichikani chochote kilichopo mbinguni wala ardhini, wala haziathiriki hukumu zake kwa matamanio ya waja na tamaa za wenye mamlaka , na miongoni mwa rehema zake ni kuwawekea sheria waja wake sheria ambazo zina maslahi kwao duniani na akhera, na kutowalazimisha katika sheria hizo jambo wasiloliweza. Na katika mambo yanayopelekea kumuabudu yeye, ni kuhukumiana katika sheria zake katika kila jambo, hilo liambatane na kuridhia toka moyoni.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Anaapa kwa nafsi Yake tukufu, kwamba hawa hawataamini kweli kweli mpaka wakufanye wewe ni hakimu kwenye ugomvi unaotokea baina yao katika uhai wako na watake uamuzi wa Sunnah yako baada ya kufa kwako, kisha wasiingiwe na dhiki katika nafsi zao kwa matokeo ya hukumu yako, na washikamane na wewe, pamoja na hivyo, kwa kukufuata kikamilifu. Kutoa uamuzi kulingana na aliyokuja nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani, kutoka kwenye Qur’ani na Sunnah katika kila jambo katika mambo ya kimaisha, pamoja na kuridhika na kusalimu amri, ni miongoni mwa uthabiti Imani”.

[An- nisaa: 65]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Je, wanataka Mayahudi hawa uhukumu kati yao kwa yale ya upotevu na ujinga waliyoyazoea washirikina wanaoabudu masanamu? Hayo hayawi wala hayafai kabisa. Na ni nani aliye muadilifu zaidi kuliko Mwenyezi Mungu katika hukumu Yake kwa aliyezifahamu sheria za Mwenyezi Mungu, akamuamini na akawa na yakini kwamba hukumu ya Mwenyezi Mungu ndiyo ya haki?”

[Al-maida 50]

About The Author