Dini ya Uislamu

Inatangazwa kupitia Dalili zitokanazo na Qur'ani na Sunnah za Mbora wa Viumbe.

Utangulizi

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi
wa Rehema Mwenye kurehemu.

Hakika kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, tunamhimidi yeye na tunamtaka msaada yeye, na tunamuomba msamaha, na tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari ya nafsi zetu, na ubaya wa matendo yetu, aliyemuongoza Mwenyezi Mungu hakuna wa kumpoteza, na aliyempoteza hakuna kipenzi wa kumuongoa, na ninashuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika wake, na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, amani na salamu nyingi.

Baada ya hayo

Leo hii Kwa hakika kuna haja kubwa ya kupatikana Kitabu kipana na kifupi, kinachoitangaza dini ya uislamu kwa ujumla wake, sawa sawa iwe ni katika mambo yanayohusu Itikadi, au Ibada, au Miamala au Adabu au mambo mengine,

Kwa kupitia kitabu hicho anaweza msomaji kujijengea fikra iliyo wazi yenye kuenea iliyokamilika kuhusu dini ya uislamu, na apate marejeo ndani ya kitabu hicho yule aliyeingia katika dini ya uislamu marejeo ya awali kabisa katika kujifunza hukumu za uislamu na adabu zake na kujifunza maamrisho yake na makatazo yake, na kipatikane kitabu hicho kwa walinganiaji katika njia ya Mwenyezi Mungu, wakikifasiri kitabu hicho katika Lugha zote, na kumpatia kila mwenye kuuliza kuhusu dini ya uislamu, na kila mwenye kuingia katika dini ya uislamu, hivyo akaongoka kwa kitabu hicho yule aliyependa Mwenyezi Mungu kuongoka kwake, na wakati huo itasimama hoja na ufikishaji dhidi ya wapingaji na waliopotoka.

Na kabla ya kuanza kuandika kitabu hiki, ni lazima kuweka njia na vigezo ambavyo atashikamana navyo mtunzi; ili aweze kufikia lengo kuu la kitabu hiki, na tunataja miongoni mwa vigezo hivyo ni haya yafutayo:

Ni kuitangaza na kuidhihirisha dini hii kwa kupitia ushahidi wa Qur’ani tukufu na Sunnah za bwana Mtume zilizotakasika, na wala siyo kupitia mifumo ya Kibinadamu ya maneno ya kubishana na kukinaishana, na kufanya hivyo ni kwa kuchunga mambo mengi:

A- Nikuwa kwa kusikiliza maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kufahamu makusudio yake anaongoka amtakaye Mwenyezi Mungu kumuongoza na husimama hoja dhidi ya mpotevu mwenye kupinga, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na pindi yeyote, miongoni mwa washirikina, akiomba kuingia kwenye himaya yako, ewe Mtume, na akataka amani, basi mkubalie maombi yake ili apate kuisikia Qur’ani tukufu na auone uongofu wake, kisha mrudishe alikotoka akiwa kwenye usalama.”

[Al-Taubah:6],

Na huenda hoja na ufikishaji usisimame kupitia usulubu wa kibinadamu na njia za maneno ambazo zimegubikwa na mapungufu.

B- Hakika Mwenyezi Mungu ametuamrisha kufikisha dini yake na wahyi wake kama alivyouteremsha, wala hakutuamrisha kuchagua njia za maneno yatokayo kwetu ili kuwaongoza watu tukidhani kuwa tutafika kwa maneno hayo kwenye nyoyo zao, kwa nini tunazisumbua nafsi zetu kwa kitu ambacho hatukuamrishwa kukifanya na tukaacha tulichoamrishwa kukifanya ?

C- Hakika njia nyingine ya Daa’wa, mfano kuwazungumzia kwa mapana kuhusu wendaji kombo wa wagomvi wetu, na kuwajibu hoja zao, katika nyanja za Itikadi au za Ibada au za Tabia au za kiadabu na uchumi, au kutumia mijadala ya kifikra na kiakili,kama kuzungumzia kuhusu kuthibitisha uwepo wa Mwenyezi Mungu- Ametukuka Mwenyezi Mungu utukufu wa hali ya juu kwa wanayomsingizia Madhalimu, au kuzungumzia mabadiliko yaliyopo katika Injili na Taurati na vitabu vya Dini zingine, na kuyaweka wazi mapungufu yake na ubatili wake.

Na yote hayo yanafaa kuwa ndiyo njia ya kuweka wazi ubovu wa misingi na Itikadi za wagomvi wetu, na inafaa vilevile iwe ni akiba ya utamaduni wa muislamu- pamoja nakuwa haimdhuru kutoijua- lakini haifai moja kwa moja kuwa ndio msingi na muelekeo ambao unasimamia ujumbe wa Mwenyezi Mungu.

D- Ni kuwa wale ambao wanaingia katika uislamu kwa kupitia njia hizi zilizokwisha tajwa, siyo lazima kuwa wao watakuwa ni waislamu wa kweli, kwani hakika anaweza kuingia mmoja wao katika dini hii kwa kupendezwa na jambo fulani ambalo limezungumzwa kwa mapana, na huenda akawa haamini mambo mengine ya msingi katika mambo ya dini, kama mwenye kupendezwa – kwa mfano- pekee uliopo katika uchumi wa kiislamu, lakini haamini maisha ya akhera, au haamini kuwepo kwa majini na mashetani na vinginevyo.

Na Aina hii ya watu madhara yao katika uislamu ni makubwa kuliko manufaa yao.

E- Hakika Qur’ani ni mtawala wa Nafsi na nyoyo, Basi ikitokea kutenganishwa Qur’ani na nafsi, basi Nafsi zilizotakasika huitafuta Qur’ani na hupanda juu katika ngazi ya Imani na uchamungu, Basi ni kwanini itenganishwe kati ya Qur’ani na Nafsi?!.

Na kusiwe na muingiliano kati ya majibu ya kivitendo, na kubanwa kwa matukio, na kutumia uzoefu wa siku nyingi katika kuitangaza na kuidhihirisha dini hii, Bali dini hii hutangazwa kama ilivyoteremka, kwa kufuata muongozo wake nao ni kuwasemesha watu na kwenda nao hatua kwa hatua mpaka kufikia hatua ya kuwa na msimamo imara.

Na azingatie sana katika uandishi kutumia mfumo mpana, na kufupisha kwa kadiri iwezekanavyo, kiasi kwamba itakuwa rahisi kukibeba kitabu hicho na kukisambaza kwa watu.

Na tufanye kuwa tumeimaliza kazi hii, na tumekitafsiri kitabu hiki, na tumekichapisha nakala milioni kumi, na kikafika kitabu katika mikono ya watu milioni kumi, na wakaziamini Aya na Hadithi zilizomo ndani ya kitabu hiki asilimia 1% miongoni mwao, na wakazikufuru na kuzipinga aya na hadithi zilizoko humo watu asilimia 99%, na ikawa hii asilimia moja ni yenye kufanya bidii na kuwa na khofu, ikitarajia Imani na uchamungu, Hivi hujui ewe ndugu yangu mtukufu kuwa hii asilimia moja katika asilimia mia moja kuwa inamaanisha kuingia watu laki moja katika Dini ya Mwenyezi Mungu?.

Na hili bila shaka ni mafanikio makubwa, Na ikiwa Mwenyezi Mungu atakuongozea mtu mmoja ni bora kwako kuliko kumiliki ngamia mwekundu.

Bali hata kama hakuamini yeyote katika hawa waliolinganiwa, na wote wakaipinga dini hii, kwa hakika tunakuwa sisi tumetekeleza amana na tumefikisha ujumbe aliotubebesha Mwenyezi Mungu.

Kwa hakika jambo la muhimu kwa walinganiaji katika njia ya Mwenyezi Mungu siyo kuwakinaisha watu kwa dini hii kwakuwa na pupa ya kuongoka kwao, kama ilivyo tajwa katika kitabu kitukufu.

“Ikiwa utafanya pupa, ewe Mtume, kuwaongoa hawa washirikina, basi jua kuwa Mwenyezi Mungu Hamuongoi mpotoshaji”

[Surat Nahli 37],

Lakini jambo lao la muhimu zaidi ni lile jambo la muhimu kwa Nabii wao alilosemeshwa na Mola wake -Aliyetakasika na kutukuka-

“Ewe Mtume, fikisha wahyi wa Mwenyezi Mungu uliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako. Na iwapo utapunguza bidii katika kuufikisha, ukaficha chochote katika wahyi huo, basi utakuwa hukuufikisha ujumbe wa Mola wako. Na Mwenyezi Mungu anakulinda na kukuokoa na maadui zako”.

[Al Maaida: 67].

Tunamuomba- Mwenyezi Mungu Mtukufu- Tuwe sote kwa pamoja ni wenye kusaidiana kufikisha Dini ya Mwenyezi Mungu kwa watu wote, na atufungulie milango ya Kheri na wenye kulingania katika mlango huo, na atufungie milango ya shari na kusimama mbele yake, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi. Na Rehema na amani ziwe juu ya Mtume Muhammad.

About The Author

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *