Dini ya Uislamu

Inatangazwa kupitia Dalili zitokanazo na Qur'ani na Sunnah za Mbora wa Viumbe.

Waislamu kutilia umuhimu misingi sahihi ya kuchukua dini hii:

ilivyo kuwa maneno na matendo na kukiri kwake Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- kumejengwa kwa maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, maneno yenye kuchambua amri zake na makatazo yake katika dini ya uislamu, Waislamu wameyatilia umuhimu mkubwa maneno hayo kutokana na usahihi ulionukuliwa kupitia hadithi zilizopokelewa kutoka kwa Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na wakatoa jitihada kubwa katika kuzisafisha nukuu kutokana na ziada ambayo si katika maneno ya Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-, na katika kubainisha kauli alizosingiziwa Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- wameweka kwa ajili hiyo kanuni madhubuti ambayo inapaswa kuchungwa katika kunakili hadithi hizi kutoka katika zama moja kwenda zama nyingine.

Na tutazungumzia kwa ufupi sana kuhusu (Elimu ya Hadithi) ili jambo hilo liwe wazi kwa msomaji, jambo hilo ambalo limeutofautisha umma wa kiislamu na mila na dini zingine, kwa kuufanyia wepesi umma wa kiislamu katika kuihifadhi dini yake na kuwa safi isiyochanganyika na uongo na uzushi katika zama zote zilizopita.

Kwa hakika dini ya uislamu imetegemea katika kunukuu maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na ya Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- Juu ya mambo mawili makubwa:

1- Kuhifadhi moyoni, na kuandika katika kurasa, na waislamu wa mwanzo ni katika umma huu walikuwa na uwezo mkubwa kuliko umma nyingi zilizopita katika kuhifadhi na kuelewa kiundani na kwa upana kwa kule kusifika kwao na sifa ya akili safi na kumbukumbu yenye nguvu, na hili linajulikana na liko wazi kwa mwenye kuisoma historia yao na wakajua habari zao, na kwa hakika alikuwa swahaba anasikia hadithi kutoka katika kinywa cha Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- na anayahifadhi vizuri na kuyanukuu kwa wakati wake, na baada yake Taabiy (mwanafunzi wa swahaba) ambaye anaihifadhi hadithi hiyo, kisha anaifikisha kwa yule aliye baada yake, na hivyo ndivyo inaendelea cheni ya hadithi mpaka kufikia kwa mmoja kati ya wasomi wa hadithi ambaye huziandika hadithi hizi na kuzihifadhi moyoni na kuzikusanya katika kitabu na kuwasomea wanafunzi wake kitabu hiki nao wanazihifadhi hizi hadithi na kuziandika kisha nao wanawasomea wanafunzi wao, na kwa mpangilio huu wakafuata na mpaka vinafika vitabu hivi katika mataifa yote wanavipata kwa njia hii na utaratibu huu.

Na kwa namna hii haikubaliki hata kidogo hadithi kutoka kwa Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- pasina kujua cheni ya wapokezi ambao imenukuliwa hadithi hii toka kwao kuja kwetu.

Na huendana na jambo hili vilevile elimu nyingine ambayo inautofautisha umma wa kiislamu na umma zingine, nayo ni elimu ya wapokezi au elimu ya Jar-hi na Taadiil.

Nayo ni elimu inayotilia umuhimu wa kujua hali za hawa wapokezi ambao wananukuu hadithi za bwana Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani – hivyo hutilia umuhimu historia yao wenyewe, kwa kujua tarehe ya kuzaliwa kwao na kufa kwao, kujua mashekhe (walimu) wao na wanafunzi wao na kuthibitishwa na wasomi wa sasa, na kujua upeo wa udhibiti wao kuwa na hifdhi nzuri, na yanayowazunguka miongoni mwa uaminifu na ukweli wa mazungumzo, na yasiyokuwa hayo katika mambo ambayo ni muhimu kwa mwanachuoni wa Hadithi ili ahakiki ukweli wa hadithi iliyopokelewa kutoka katika mlolongo wa wapokezi.

kwa hakika hiyo ni elimu ya kipekee katika umma huu kwa kuipupia juu ya usahihi wa maneno yaliyo egemezwa kwa Mtume wa umma huu, na wala haipatikani katika Historia nzima kuanzia mwanzo mpaka leo juhudi kama hii kubwa ya kutilia umuhimu maneno ya mtu yeyote kama yalivyotiliwa umuhimu maneno ya Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani -.

Hakika hiyo ni elimu kubwa iliyonukuliwa katika vitabu vilivyotilia umuhimu uliotimia katika kupokea hadithi, na imetaja historia binafsi kwa mchanganuo kwa maelfu ya wapokezi, siyo kwa ajili ya chochote isipokuwa ni kwa sababu wao walikuwa ni kiunganishi katika kuhamisha hadihi za Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani – kuzipeleka kwenye zama zinazofuata, na katika elimu hii hapakuwa na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa kwa mtu yeyote, bali elimu hiyo ilikuwa kama mizani kina cha ukosoaji, muongo huambiwa kuwa ni muongo, na mkweli huitwa mkweli na mwenye hifdhi mbaya huambiwa na mwenye hifdhi imara huambiwa vilevile, kwa hivyo, na wakaiwekea elimu hiyo ya Jarhi wa Taadiil misingi kabambe ambayo wanaijua watu wa fani hii.

Na wala haiwi hadithi sahihi kwao isipokuwa itakapoungana cheni ya wapokezi walioipokea wao kwa wao, na ukatimia uadilifu wa hawa wapokezi na ukweli wa maneno pamoja na nguvu ya hifdhi na udhibiti.

Jambo jingine katika elimu ya hadithi.

Ni katika ongezeko la mlolongo wa cheni wa hadithi moja, pale ambapo inafikia hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani- kuwa na njia nyingi na milolongo ya wapokezi, hivyo basi inakuwa hadithi moja ina cheni mbili au tatu au Nne na wakati mwingine inakuwa na cheni kumi na wakati mwingine zaidi ya hapo.

Na kila unavyo ongezeka mlolongo wa cheni ya mapokezi ya hadithi ndivyo inavyokuwa hadithi ina nguvu zaidi, na kuzidi kuwa madhubuti katika tabaka zake zote na ikiwa hivyo huitwa Hadithi Mutawaatir (Mfululizo) nayo ni aina ya juu zaidi ya nukuu kwa waislamu, na kila ambavyo jambo linakuwa muhimu zaidi katika dini ya uislamu kama kuweka wazi nguzo za uislamu basi huwa Hadithi mutawaari zinakuwa nyingi katika kuelezea jambo hilo, na huongezeka cheni zake za upokeaji, na kila inapokuwa jambo ni la matawi na mambo yenye kupendeza zinakuwa chache cheni za mapokezi yake na utiliwaji muhimu wake unakuwa ni hafifu.

Na Daraja la juu zaidi ambalo waislamu walilipa kipaumbele katika usahihi wa kunukuu ni kunukuu Qur’ani Tukufu pale ambapo ilipata kutiliwa umuhimu wa hali ya juu kwa kuandikwa katika makaratasi na kuhifadhiwa vifuani, na kuyaboresha matamshi yake na matokeo ya herufi zake na njia za usomaji wake, na kwa hakika waislamu waliinukuu kwa mlomlongo wa maelfu ya mapokezi kupitia vizazi na vizazi, hivyo haikuwezekana kuingiliwa na mkono wa upotoshaji na ubadilishaji kwa miaka yote iliyopita, na msahafu ambao unasomwa Magharibi ndiyo msahafu unaosomwa mashariki. Ndiyo msahafu uliopo katika sehemu mbalimbali za ardhi, kwa kusadikisha maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Hakika sisi tumeiteremsha Qur’ani na hakika sisi tunachukua ahadi kuihifadhi”.

About The Author