Nguzo za Uislamu
Uislamu una nguzo tano za msingi, kwa uwazi wake nikuwa ni wajibu wa muislamu kulazimiana na nguzo hizo mpaka isadikike kwake kuwa na sifa ya kuitwa muislamu.
1- Ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake na muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Na ni neno la kwanza ambalo anapaswa aliseme mwenye kuingia katika uislamu, na atasema: (Ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan rasuulullah)- Nashuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kuwa Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu-aseme maneno hayo akiamini maana zake zote, kama tulivyo fafanua huko nyuma.
Basi anaitakidi kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola mmoja wa pekee ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa, wala hana yeyote mwenye kufanana naye, na yeye ndiye muumba na asiye kuwa yeye basi huyo ni kiumbe, na yeye peke yake ndiye Mwenyezi Mungu anayestahiki kuabudiwa, hakuna mola mwingine asiyekuwa yeye, na anaitakidi kuwa Muhammad ni mja wa Mwenyezi Mungu na ni Mtume wake aliyeteremshiwa wahyi kutoka mbinguni na mfikishaji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wa maamrisho yake na makatazo yake ni wajibu kumsadikisha katika yale aliyoyatolea habari na kumtii katika yale aliyoyamrisha na kujiepusha na yale aliyoyakataza na kuyakemea.
B- Nguzo ya pili: Kusimamisha swala.
Na katika Sala kuna dhihiri alama za unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na mja husimama hali yakuwa mnyenyekevu anasoma aya za Qur’ani na kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa aina tofauti za Dhikri na sifa, akirukuu kwa ajili yake na akaporomoka hali ya kusujudu, akimnong’oneza na kumuomba na kumtaka kutokana na fadhila zake tukufu na hayo ni kiunganishi kati ya mja na Mola wake ambaye amemuumba na anajua mambo yake ya siri na dhahiri na kumuelekea Mwenyezi Mungu mja wake wakati wa kusujudu, kufanya hivyo ni sababu ya kumpenda Mwenyezi Mungu mja wake na kuwa karibu naye na kumridhia, na mwenye kuacha ibada kwa kiburi cha kuacha kumwabudia Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humkasirikia na humlaani na hutoka mtu huyo katika uislamu.
Na wajibu ni kusali sala tano kwa kila siku ikikusanya ndani yake kisimamo na kusoma suratil faatiha:
Naanza kusoma Qur’ani kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewaenea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemevu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama inavyonasibiana na haiba Yake.
Shukrani zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema mwenye kurehemu
Mwingi wa rehema na mwenye kurehemu.
Na Yeye, kutakasika ni Kwake, Peke Yake Ndiye Mwenye mamlaka ya Siku ya Kiyama, nayo ni Siku ya Malipo kwa matendo yaliyofanywa na waja. Muislamu anapoisoma aya hii katika kila rakaa, inamkumbusha siku ya Akhera na inamhimiza ajitayarishe kufanya matendo mema na kujiepusha na maasia na mabaya.
Wewe tu ndiye tunayekuabudu na wewe tu ndiye tunayekuomba msaada.
Tuongoze njia iliyonyooka.
Njia ya wale uliowaneemesha. Na siyo ya wale waliokasirikiwa, wala ya waliopotea
Suratul- Faatiha 1-7
Na kusoma chochote chepesi katika Qur’ani na ikijumuisha kurukuu na kusujudu na kumuomba Mwenyezi Mungu na kumtukuza kwa kusema:- Allahu Ak-bar- (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa) na kwenye kurukuu kwa kusema :- Sub-hana rabbiyal Adhwiim- (Ametakasika Mola wangu Mtukufu) na kwenye kusujudu kwa kusema (Sub-haana rabbiyal Aala) ametakasika Mola wangu aliye juu.
Na kabla ya kutekeleza ibada ya sala ni lazima kwa mwenye kusali awe amejitwaharisha kutokana na najisi (haja ndogo na haja kubwa) katika mwili wake na mavazi yake na sehemu yake ya kusalia, awe ametawadha kwa maji na huko kutawadha kuna kuwa kwa kuosha uso wake na mikono yake na kupaka kichwa chake maji kisha kuosha miguu yake miwili.
Na kama atakuwa ni mwenye janaba (kwa kuingiliana na mke wake) basi ni wajibu juu yake kuoga kwa kuuosha mwili wake wote.
C- Nguzo ya Tatu: ZAKAH.
Nacho ni kiwango fulani cha rasilimali amekifaradhisha Mwenyezi Mungu kwa matajiri kuwapa mafukara na masikini na wenye kuhitajia miongoni mwa watu katika jamii ili kukidhi mahitajio yao na idadi yake kifedha ni asilimia mbili na nusu katika mia moja, kutoka katika rasilimali, na hugawiwa kwa mwenye kustahiki Zakah.
Na nguzo hii ni sababu ya kuenea misaada ya kijamii kati ya mtu mmoja mmoja katika jamii pamoja na kuzidisha mapenzi na kuzoeana na kusaidizana baina yao na kuondosha chuki na vifundo kutoka katika tabaka la masikini kwenda kwenye tabaka la matajiri na waliofanyiwa wepesi, na ni sababu kuu ya kukuwa kwa uchumi na kuendelea kwa mzunguko wa mali kwa mfumo sahihi na kufika kwenye tabaka zote za jamii.
Na hizi Zakkah ni wajibu katika mali kwa aina zote za mali, kuanzia pesa na wanyama na matunda na nafaka na mali iliyoandaliwa kwa ajili ya kuuzwa na zisizokuwa hizo kwa viwango tofauti kutokana na rasilimali ya kila aina katika aina za mali.
D- Nguzo ya Nne : Kufunga Mwezi wa Ramadhani
Swaumu: Kufunga ni kujizuilia na kula na kunywa na kuwaendea wake, kwa nia ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, kujizuia kuanzia kuchomoza Alfajiri mpaka kuzama jua.
Na Mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao Mwenyezi Mungu amefaradhisha kufunga katika mwezi huo, ni Mwezi wa Tisa katika miezi ya miandamo, nao ni mwezi ambao ilianza kushuka Qur’ani kwa Mtume-Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao imeshuka ndani yake Qur’ani hali ya kuwa ni muongozo wa watu na wenye kutenganisha kati ya haki na batili, basi yeyote atakaye kuwepo wakati mwezi huo unaandama basi na afunge mwezi huo}
[Al Baqara: 185].
Na miongoni mwa faida kubwa za funga nikujizoesha kusubiri na kuongeza nguvu ya uwezo wa uchamungu na imani katika moyo, na hivyo ni kuwa swaumu ni siri kati ya mja na Mola wake kwani mwandamu anaweza kujitenga akakaa sehemu akala na akanywa na wala asijue mtu yeyote kufunga kwake, basi ikiwa ataacha kufanya hivyo kwa ajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu na kutii amri zake peke yake asiye na mshirika na yeye akijuwa kuwa hakuna yeyote anayeweza kuiona ibada yake hii isipokuwa Mwenyezi Mungu, inakuwa hiyo ni sababu ya kumzidishia imani na ucha mungu wake, na kwa hivyo ndiyo ikawa malipo ya wenye kufunga ni makubwa kwa Mwenyezi Mungu, bali wana mlango maalumu peponi uitwao mlango wa Rayyan.
Na muislamu anatakiwa kufunga swaumu za hiyari kwa ajili kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu, zisizokuwa za Mwezi wa Ramadhani siku zote za mwaka mzima isipokuwa siku mbili za Eid ulfitri na Eidul adh-ha.
E- Nguzo ya Tano: Ni kuhiji nyumba tukufu.
Na ni lazima kwa muislamu kuitekeleza mara moja katika umri wake wote, na kama atazidisha zaidi ya mara moja basi itakuwa ni kujikurubisha zaidi kwa Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu.
“Na Mwenyezi Mungu amewawajibishia watu wafanye hijja kwenye nyumba hiyo tukufu kwa mwenye kuweza kufunga safari ya kwenda huko”.
[Al-Imran: 97].
Basi atasafiri muislamu kwenda katika viwanja vya ibada katika mji Mtukufu wa Makka katika mwezi wa Hijja nao ni mwezi wa mwisho katika miezi ya Hijriya mwezi mwandamo, na kabla ya kuingia Makkah atavua muislamu nguo zake na atavaa vazi la Ihraam nazo ni shuka mbili nyeupe.
Kisha atafanya matendo mbali mbali ya Hijja ikiwemo kutufu nyumba tukufu Alkaaba na kufanya Saayi -kukimbia- baina ya Mlima Swafaa na Mar-waa na kusimama Arafa na Kulala Muzdalifah na kufanya matendo mengine.
Na Hijja ni mkusanyiko mkubwa wa waislamu Duniani unawafunika udugu na kuhurumiana na pamoja na kupeana nasaha, vazi lao ni moja na kiwanja chao ni kimoja hakuna yeyote kati yao anayekuwa mbora isipokuwa kwa uchamungu, na malipo ya Hijja ni makubwa, amesema Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani:
{Yeyote atakaye Hijji na akawa hakuzungumza upuuzi wala kufanya machafu, ataondoka kwenye madhambi nakuwa kama siku alivyozaliwa na mama yake} (4)
(4) Hadithi hii ameitoa Imamu Bukhariy na Muslimu(2/164) Kitabu cha Hijja ,mlango wa ubora wa hijaa iliyotimia.