Dini ya Uislamu

Inatangazwa kupitia Dalili zitokanazo na Qur'ani na Sunnah za Mbora wa Viumbe.

Mambo yaliyo haramu na yaliyokatazwa.

Jambo la Kwanza: Shirki; Kuelekeza aina yoyote katika aina za ibada kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu)

Kama mwenye kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu au kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kumtaka amkidhie haja zake au achinje kikurubisho kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, sawa sawa awe huyu anayeombwa yuko hai au amekufa au kaburi au sanamu au jiwe au mti au Malaika au walii au mnyama au visivyokuwa hivyo vilivyotajwa, yote hayo ni shirki ambayo Mwenyezi Mungu hamsamehe mja isipokuwa akitubia na akaingia katika uislamu upya.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Hakika Mwenyezi Mungu, Hamsamehe aliyemshirikisha Yeye na yeyote miongoni mwa viumbe Wake au akamkufuru kwa aina yoyote ya ukafiri mkubwa. Lakini Anayasamehe na kuyafuta madhambi yaliyo chini ya ushirikina kwa Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na yeyote anayemshirikisha Mwenyezi Mungu na mwingine, hakika amefanya dhambi kubwa”.

[Al- nisaa :48]

Hivyo Muislamu hamuabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu -kutakasika na machafu ni kwake- na wala hamuombi isipokuwa Mwenyezi Mungu na wala hamnyenyekei isipokuwa Mwenyezi Mungu amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Sema, «Hakika Swala yangu na kuchinja kwangu wanyama, na uzima wangu na kufa kwangu vyote ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu muumba wa walimwengu wote”.

«Asiye na mshirika katika uungu Wake wala katika umola Wake wala katika majina Yake na sifa Zake. Kumpwekesha huko Mwenyezi Mungu kulikosafishika ndiko Alikoniamrisha mimi Mola wangu, Aliyetukuka na kuwa juu. Na mimi ni wa kwanza kumfuata Mwenyezi Mungu kikamilifu katika umma huu.»

[Surat An-aam 162-163]

Na miongoni mwa shirki vilevile: ni kuitakidi kuwa Mwenyezi Mungu ana mke au mtoto -ametukuka Mwenyezi Mungu na kaepukana na hayo kutukuka kukubwa- au kuitakidi kuwa kuna mungu mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye anaendesha ulimwengu huu.

«Lau mbinguni na ardhini kungekuwa na waungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, wenye kuyaendesha mambo yake, ungeliharibika mpango wake. Basi Mwenyezi Mungu, Bwana wa ‘Arshi, Ameepukana na sifa za upungufu na Ametakasika na kila sifa ambayo wakanushaji makafiri wanamsifu nayo ya uongo, uzushi na kila aibu”.

[Al-anbiyau 22]

Jambo la pili: Uchawi, Ukuhani, na kudai kujua mambo yaliyofichikana:

Uchawi na ukuhani ni Kufuru, na wala mchawi hawezi kuwa mchawi isipokuwa kwa kuwa na mawasiliano na mashetani, na kuwaabudu kinyume na Mwenyezi Mungu, hivyo basi haifai kwa muislamu kwenda kwa mchawi na wala haifai kuwasadikisha katika uongo wao wa kudai kujua mambo yaliyofichikana, na katika mambo ambayo wanayatolea habari katika matukio na habari ambazo wanadai kuwa zitatokea baadaye.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Sema, ewe Mtume, kuwaambia wao, «Hakuna yeyote ajuwaye, mbinguni wala ardhini, jambo lolote lililofichikana ambalo Mwenyezi Mungu Amejihusisha Mwenyewe kulijua. Na wao hawajui ni lini watafufuliwa kutoka makaburini mwao wakati wa Kiyama kusimama.»

[An-namlu 65]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, ni mjuzi wa kisichoonekana na macho. Hatakitoa wazi hicho kisichoonekana kwa yeyote miongoni mwa viumbe Wake”.

Isipokuwa kwa yule Aliyemchagua Mwenyezi Mungu na kumpendelea kwa kumpa utume, kwani Yeye huwajuza baadhi ya yale yaliyofichika yasionekane. Na Anatuma, mbele ya huyo Mtume na nyuma yake, Malaika wenye kumhifadhi na majini, ili wasiisikilize kwa kuiba jambo hilo la ghaibu, kisha wakaambiana kwa siri kisha wakawadokeza makuhani”.

[Al Jinni: 26-27].

Jambo la Tatu: Dhulma:

Na Dhulma ni mlango mpana, yanaingia humo matendo mengi mabaya na sifa mbaya ambazo zinamuathiri mtu mmoja mmoja, inaingia ndani yake mtu kujidhulumu yeye mwenyewe nafsi yake na kumdhulumu aliye pembezoni mwake, na kuidhulumu jamii yake, bali na kuwadhulumu maadui wake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutokuwafanyia uadilifu fanyeni uadilifu huko ndiko kunako mkurubisha mtu na uchamungu}

[Al Maaida: 8].

Na kwa hakika ametueleza Mwenyezi Mungu kuwa yeye hawapendi madhalimu. Amesema Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-

(Enyi waja wangu hakika mimi nimeharamisha Dhulma katika nafsi yangu na nimeifanya kuwa haramu baina yenu hivyo msidhulumiane) (24).

Amesema Mtume rehema za mwenyezi mungu ziwe juu yake na amani:

“Msaidie ndugu yako akiwa amedhulumu au kudhulumiwa”, Akasema mtu mmoja: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unaonaje ikiwa ndugu yangu kadhulumu, vipi nitamsaidia? Akasema: “Unamuhama au unamzuia asifanye Dhulma, kwa kufanya hivyo ndiyo kumnusuru” [25]

[24] ameitoa muslim: Kitabu cha wema na kuunga udugu,mlango wa kuharamisha Dhulma(16/132)

[25] Ameitoa Bukhariy katika kitabu cha Dhulma na hasira ,mlango unaohusu kumnusuru ndugu yako dhalimu au mdhulumiwa: (3/168)

Jambo la Nne: Kuua Nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha kuiua isipokuwa kwa haki:

Nalo ni kosa kubwa sana katika dini ya uislamu, na Mwenyezi Mungu ameahidi adhabu kali kwa atakaye fanya kosa hilo na akaliwekea adhabu kali duniani nayo ni kuuliwa mwenye kuuwa, isipokuwa atakaposamehe ndugu wa aliyeuliwa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{kwa sababu hiyo tuliwafaradhishia wana wa Israeli, yakwamba yeyote atakayeua nafsi bila ya hatia au akafanya ufisadi katika ardhi, atakuwa ni kama amewauwa watu wote, na atakayeihuisha basi atakuwa ni kama amewahuisha watu wote}.

[Al Maaidah: 32].

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na mwenye kumfanyia uadui Muumini akamuua kwa kusudi pasi na haki, mwisho wake atakaoishia ni Jahanamu, hali ya kukaa milele humo, pamoja na kukasirikiwa na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kufukuzwa kwenye rehema Yake, iwapo Mwenyezi Mungu Atamlipa kwa kosa lake. Na Mwenyezi Mungu Amemuandalia adhabu kali zaidi kwa uhalifu huu mkubwa aliyoufanya. Lakini Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, Atawasamehe na kuwafadhili wenye Imani kwa kutowapa malipo ya kukaa milele ndani ya Jahanamu”.

[An-nisaa 93]

Jambo la Tano: Kuwavamia watu katika mali zao:

Sawa iwe kwa wizi au kupokonya au kwa Rushwa au kwa utapeli au kwa njia nyingine zisizokuwa hizo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na mwizi wa kiume na mwizi wa kike, wakateni, enyi watawala, mikono yao kuambatana na Sheria. Hayo yakiwa ni malipo yao kwa kuchukua kwao mali ya watu pasi na haki, na ni mateso ambayo kwayo Mwenyezi Mungu Anawazuia wengineo kufanya mfano wa kitendo chao. Na Mwenyezi Mungu ni Mshindi katika mamlaka Yake, ni Mwenye hekima katika amri Zake na makatazo Yake”.

[Al-maaida 38]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Na wala msile mali zenu baina yenu kwa Batili}

[Al-baqara 188]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Wale wanaozifuja mali za mayatima wakawa wanazichukua pasi na haki, hakika wanakula Moto utakaowaka matumboni mwao Siku ya Kiyama; watauingia Moto ambao watalisikia joto lake”.

[An Nisaa: 10].

Hivyo uislamu unapiga vita kwa nguvu uadui wa mali za watu wengine, na umetilia mkazo sana jambo hilo, na umempangia mwenye kufanya uadui wa mali za watu adhabu nzito ambayo ni kemeo kwake na watu mfano wake wenye kuvunja nidhamu na amani katika jamii.

Jambo la sita: Kughushi na kusaliti na kufanya hiyana:

Katika miamala yote kuanzia kuuza na kununua na makubaliano na mambo mengine, nazo ni sifa mbaya ambazo uislamu umezikataza na kuzitahadharisha sifa hizo.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Adhabu kali ni ya wale wanaopunja vipimo vya vibaba na mizani”.

Ambao wakinunua kwa watu cha kupimwa kwa vibaba au kwa mizani hujikamilishia wao wenyewe.

Na wakiwauzia watu kinachouzwa kwa vibaba au mizani wanapunguza vipimo.

Hivi hawadhanii kuwa wao watafufuliwa?

katika Siku kubwa?

Siku watakaposimama watu mbele ya Mweyezi Mungu ili Awahesabu kwa machache na mengi waliyoyatenda.

[Al Mutwaffifiin: 1-5].

Amesema Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake:

{Yeyote atakaye tufanyia ghushi (udanganyifu) huyo si katika sisi}

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Hakika Mwenyezi Mungu hampendi yeyote yule mwenye sifa ya hiyana mwenye madhambi}

[An- nisaa 107]

(26) hadith ameitoa muslim : kitabu cha imani ,mlango wa wa maneno ya mtume)(yeyote atakae fanya ghishi siyo katika sisi)(2/109)

Jambo la saba: Kuwashambulia watu:

Kuwashambulia katika heshima zao kwa kuwatukana na kuwasengenya na kuwafitinisha na kuwahusudu na kuwadhania vibaya na kuwapeleleza, na kuwadharau, na mengine yasiyokuwa hayo, unachunga sana uislamu kujenga jamii iliyosafi na twahara inayogubikwa na upendo na udugu na uaminifu na kusaidiana, na ndiyo sababu uislamu unapiga vita kwa nguvu maradhi yote ya kijamii ambayo yanapelekea mpasuko katika jamii na kueneza chuki na ugomvi na umimi kati ya watu wake.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kwa vitendo, wasitoke wanaume Waumini wakawacheza shere wanaume Waumini wengine, huenda akawa yule anayechezwa shere katika wao ni bora kuliko wale wenye kucheza shere, na wasitoke wanawake Waumini wakawacheza shere wanawake Waumini wengine, kwani huenda yule anayechezwa shere miongoni mwao ni bora kuliko wale wenye kucheza shere. Wala msitiane dosari nyinyi kwa nyinyi, wala msiitane majina ambayo yanachukiwa na wenye kuitwa nayo, kwani ubaya wa sifa na jina ni utokaji nje wa maadili ya Dini, nao ni kucheza shere kwa njia ya dharau, kuaibisha kwa maneno au ishara na kupeana majina mabaya, baada ya kuwa mmeingia kwenye Uislamu na mmeufahamu. Na Asiyetubia na huku kuchezeana shere, kutiana dosari, na kuitana majina mabaya na utokaji nje wa maadili ya Dini, basi hao ndio watu waliozidhulumu nafsi zao kwa kuyatenda mambo haya yaliyokatazwa”.

“Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo, Jiepusheni na dhana mbaya nyingi kwa Waumini, kwani dhana nyingine ni dhambi. Wala msipekue aibu za Waislamu, wala msisemane nyinyi kwa nyinyi maneno yenye kuchukiwa na wenye kusemwa na hali wao hawapo. Je, anapenda mmoja wenu kula nyama ya ndugu yake akiwa amekufa? Nyinyi mnalichukia hilo, basi lichukieni lile la kumsengenya. Na muogopeni Mwenyezi Mungu katika yale Aliyowaamrisha nyinyi na kuwakataza. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba za waja Wake Waumini, ni Mwingi wa rehema kwao”.

[Al-hujuraat 11-12]

Kama ambavyo uislamu unapiga vita kwa nguvu kubwa kufarakana na matabaka na kujipambanua kitabaka kati ya watu wa jamii moja kwa watu wote, kila mtu kwa mtazamo wa uislamu ni sawa, hakuna ubora kwa mwarabu na asiyekuwa mwarabu wala ubora wa mweupe kwa mweusi isipokuwa ubora unakuwa kwa kile mtu alichokibeba katika moyo wake katika mambo ya dini na uchamungu, watu wote hushindana kwa mipaka iliyosawa katika matendo mema. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Enyi watu! Sisi tumewaumba nyinyi kutokana na baba mmoja, naye ni Ādam, na mama mmoja, naye ni Ḥawā’, hivyo basi hakuna kufadhilishana baina yenu kinasaba, na tumewafanya nyinyi kwa kuzaana kuwa mataifa na makabila mbalimbali ili mjuane nyinyi kwa nyinyi, hakika mtukufu wenu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule anayemcha Yeye zaidi. Hakika Mwenyezi Mungu Anawajua sana wachamungu na Anawatambua”.

[Alhujuraat 13[Al Hujrati: 13].

Jambo la Nane: Kucheza Kamari na kunywa pombe na kutumia madawa ya kulevya:

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Enyi mlioamini Hakika pombe na kamari na kuabudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu na kutazamia kwa mishale ya kupiga ramli ni uchafu na ni katika kazi za shetani basi jiepusheni navyo ili mpate kufaulu }

Hakika Shetani anataka, kwa kuwapambia madhambi, kuweka baina yenu chenye kuleta uadui na chuki, kwa sababu ya kunywa pombe na kucheza kamari, na kuwaepusha na kumtaja Mwenyezi Mungu na kuswali, kwa kutokuwa na akili katika unywaji pombe na kujishughulisha na pumbao la uchezaji kamari. Basi komekeni na hayo.

[Al Maida: 90-91].

Jambo la tisa: Ni kula nyamafu, na damu na nyama ya nguruwe:

Na vitu vyote vichafu ambavyo vina madhara kwa mwanadamu, na vilevile vichinjwa vinavyokurubishwa siyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Enyi Waumini, kuleni katika vyakula mnavyovipenda vilivyo halali ambavyo tumewaruzuku, wala msiwe kama makafiri ambao wanaviharamisha vizuri na kuvihalalisha viovu na mumshukurie Mwenyezi Mungu neema Zake kubwa kwenu kwa nyoyo zenu, ndimi zenu na viungo vyenu, iwapo kwa kweli nyinyi mnafuata amri Yake, ni wenye kusikia na kumtii Yeye, mnamuabudu Yeye Peke Yake Asiyekuwa na mshirika”.

“Hakika Mwenyezi Mungu Amewaharamishia nyinyi kinachowadhuru, kama mfu ambaye hakuchinjwa kwa njia ya kisheria, na damu inayotiririka, na nyama ya nguruwe, na vichinjwa ambavyo vilikusudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Na katika wema wa Mwenyezi Mungu na usahilishaji Wake kwenu ni kwamba Amewahalalishia nyinyi kuvila vitu hivi vilivyoharamishwa wakati wa dharura. Hivyo basi, yeyote ambaye dharura itampelekea kula kitu katika hivyo, pasi na kuwa ni mwenye kudhulumu katika kula kwake kwa kupitisha kipimo cha haja yake, wala kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu katika yale aliyohalalishiwa, basi huyo hana dhambi kwa hilo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe waja Wake, ni Mwenye huruma kwao”.

[Al-baqara 172-173]

Jambo la kumi: Kufanya zinaa na Tendo la watu wa Nabii Luti (kuingiliana nyuma):

Uzinifu ni katika kitendo kichafu chenye kuharibu tabia na jamii na husababisha mchanganyiko katika nasaba na kupoteza familia, na kukosa malezi sahihi, na watoto wa zinaa ndiyo wanaohisi uchungu wa uovu na kuichukia jamii. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Wala msikaribie uzinifu na mambo yanayopelekea huko ili msiingie ndani yake, hakika hilo ni tendo baya sana, na njia mbaya zaidi ni njia ya tendo hilo”.

[Al-israa 32]

Na hiyo zinaa ni sababu ya kuenea magonjwa ya jinsia yenye kuangamiza nguvu kazi ya jamii. Amesema Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-

{Hautaenea uchafu kwa watu mpaka kufikia hatua ya kuutangaza uchafu huo, isipokuwa malipo yake yatakuwa ni kuenea maradhi ya milipuko na maradhi mengine ambayo hayakuwepo kwa waliotangulia kabla yao}(27)

(27) Hadithi ameitoa ibnu majjah :kitabu cha fitina mlango wa makosa (2/1333)na amesema Al-baniy kuhusu hadithi hiyo kuwa ni hasan(swahhi ibnu majjah(2/370)

Na kwa hivyo basi ameamrisha Mwenyezi Mungu kuziba mianya yote yenye kupelekea kufanya zinaa, basi akawaamrisha waislamu kuinamisha macho yao kwa sababu kutazama haramu ndiyo chanzo cha kupelekea kwenye uzinifu, na akawaamrisha wanawake kujisitiri na kuvaa Hijabu na kujilinda na uzinzi, ili kuilinda jamii kutokana na uchafu wa zinaa, na kwa upande mwingine uislamu ukaamrisha kuoa na kuhimiza kuoa na kupendezesha kuoa bali umeahidi malipo makubwa na thawabu hata kwa kustarehe kwa tendo la ndoa ambalo wanalifanya mume na mke, hayo yote ili kuanzisha familia yenye heshima na yenye kujihifadhi na kutofanya machafu, ili iwe ni kitovu cha malezi yenye mafanikio katika kumlea mtoto wa leo ambaye atakuwa kijana wa kesho.

Jambo la kumi na moja: Kula Riba :

Riba ni maangamizi ya uchumi na kuchukua fursa ya mwenye kuhitajia mali, sawa sawa awe mfanya biashara katika biashara yake au fakiri mwenye kuhitajia, na riba ni kukopesha mali mpaka ufikie muda fulani kwa kutoa badala yake ziada fulani wakati wa kuilipa ile mali, hivyo basi mkopeshaji anatumia fursa ya kuhitajia mali kwa fakiri, na anabeba mzigo mkubwa wa madeni yaliyolimbikizana zaidi ya alichopewa.

Na mtoa riba anatumia fursa ya uhitaji wa mfanya biashara au viwanda au wakulima au wengine wasiokuwa hao miongoni mwa wenye kuendesha uchumi.

Anatumia fursa ya uhitaji wao wa lazima kuwaelekeza kwenye mtiririko wa pesa, na kuwawekea kiwango cha ziada ya faida katika kile walichokikopa, bila wao (wakopeshaji) kuhusika katika kile kitakachotokea miongoni mwa hatari kama kufilisika au kupata hasara.

Na akipata hasara huyu mfanya biashara hulimbikizana madeni na humtupia deni hilo mtoa riba, wakati ambapo wangekuwa ni wenyekushirikiana katika faida na hasara, huyu angeshiriki kwa juhudi zake na huyu kwa mali zake kama ulivyoamrisha uislamu, lingezunguka gurudumu la uchumi endelevu kwa maslahi ya wote.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na mkamfuata Mtume Wake, muogopeni Mwenyezi Mungu na muache kutaka ziada iliyosalia juu ya rasilimali zenu, ambayo mlistahiki kupata kabla riba haijaharamishwa, iwapo imani yenu ni ya dhati kimaneno na kivitendo”.

Msipokomeka na hilo mlilokatazwa na Mwenyezi Mungu, basi kuweni na yakini ya vita kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na mkirudi kwa Mola wenu na mkaacha kula riba, ni haki yenu mchukue madeni yenu bila ya nyongeza, msimdhulumu yeyote kwa kuchukua zaidi ya rasilimali zenu wala msidhulumiwe na yeyote kwa kupunguza kiwango cha pesa mlichokopesha”.

Na iwapo mdaiwa hawezi kulipa, mpeni muhula mpaka Mwenyezi Mungu Atakapomfanyia sahali (wepesi) riziki na kuwarudishia mali yenu. Na mkiacha rasilimali yote au baadhi yake mkamuondolea mdaiwa, hilo ni bora zaidi kwenu, mkiwa mnajua fadhila yake ya kuwa hilo ni bora kwenu katika ulimwengu na Akhera”.

[Al Baqara: 278-279].

Jambo la kumi na mbili: uchoyo na ubahili:

Nao ni dalili ya umimi na kujipendelea mwenyewe, na kwa ubahili huu anakuwa ni mwenye kulimbikiza mali na kukataa kuitolea zakah kwa ajili ya kuwapa mafukara na maskini, na anapingana na jamii yake kwa kukataa vyanzo vya kusaidiana na kujenga udugu ambao ameuamrisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na Wala wasidhani wale wanaozifanyia ubahili neema za Mwenyezi Mungu Alizowaneemesha kwa kuwafadhili kwamba ubahili huo ni bora kwao. Bali hiyo ni shari kwao. Kwani mali hiyo waliyoikusanya itakuwa ni kitanzi cha moto kitakachowekwa shingoni mwao Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ndiye Mwenye kumiliki ufalme; na Yeye Ndiye Atakayesalia baada ya kutoweka viumbe Wake wote. Yeye Ndiye Mtambuzi wa matendo yenu yote, na Atamlipa kila mtu kwa kadiri anavyostahiki.

[Al-Imran: 180].

Jambo la kumi na tatu: Uongo na kutoa ushahidi wa uongo:

Na kwa hakika tulitanguliza kauli ya Mtume Rehema za Allah ziwe juu yake na amani

“Na Tahadharini sana na uongo! kwani uongo unapelekea katika uovu, na hakika uovu unampelekea mtu kuingia Motoni, na hatoacha mtu kuendelea kusema uongo, na kuutafuta uongo mpaka ataandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni muongo”.

Na miongoni mwa uongo wenye kuchukiza ni ule ambao unakuwa wakati wa kutoa ushuhuda wa uongo, na kwa hakika alitilia mkazo Mtume -Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani – katika kuwaweka mbali watu na kushuhudia uongo na akatahadharisha kwakuwa mwisho wake ni mbaya, na akainua sauti yake kwa kuwaambia maswahaba zake:

“Hivi nisikufahamisheni dhambi kubwa zaidi, ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kutowatendea wema wazazi wawili”, na alikuwa ameegemea akakaa na akasema: “Eleweni vyema pia na kuzungumza uongo, eleweni vyema pia na kutoa ushuhuda wa uongo”. [28]

Na hakuacha kurudiarudia kwa kutahadharisha umma usijekuangukia katika kusema na kushuhudia uongo.

(28) hadithi ameitoa bukhari kitabu cha ushuhuda ,mlango wa uliosemwa katika kushuhudia uongo(3/225)

Jambo la kumi na Nne: Kiburi na kudanganyika, kujisikia na majivuno:

Kiburi na kudanganyika na majivuno, ni sifa mbaya na dharau zenye kuchukiwa katika dini ya uislamu, na kwa hakika ametuhabarisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa yeye hawapendi wenye viburi, na akasema kuhusu wao huko akhera.

{Hivi haikuwa jahanamu ndiyo mafikio ya wenye kufanya kiburi} [Azzumar 60]

About The Author