Kipenzi changu msomaji.
Kitabu hiki ambacho kiko mikononi mwako kinakufahamisha kuhusu uislamu, kwa Taswira pana na iliyoenea sehemu zake zote (Itikadi zake, Adabu, Sheria na Mafunzo yake yote).
Na kwa hakika nimechunga mambo mengi ya msingi katika kitabu hicho:
La Kwanza: Kutilia umuhimu misingi ya dini ambayo dini imesimama kwa misingi hiyo.
La Pili: Kufupisha kwa kadiri iwezekanavyo.
La Tatu: Kuutangaza uislamu kupitia vyanzo vyake asili (Qur’ani tukufu, Hadithi za Bwana Mtume- Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na amani-) pale ambapo msomaji anasimama moja kwa moja mbele ya Chemchem ya misingi ya uislamu akinywa moja kwa moja muongozo wake na mafundisho yake kutoka katika chemchem.
Na utakuta ewe kipenzi changu msomaji, baada ya kufika mwisho wa kitabu hiki, kuwa imejengeka kwako fikra iliyowazi kuhusu dini ya uislamu, kiasi kwamba utaweza baada ya hapo kupanda ngazi katika kuinua akiba ya elimu kuhusu dini hii.
Hakika kitabu hiki ambacho kiko mikononi mwako ni muhimu kwa kundi kubwa la watu, na kinawapa kipaumbele kwa daraja la kwanza wale wenye mapenzi makubwa ya kuingia katika uislamu, na kujifunza Itikadi zake na adabu zake na hukumu zake.
Kama ambavyo kinatoa kipaumbele kwa wenye kutilia umuhimu wa kuzitambua dini mbalimbali ambazo zinakimbiliwa na Mamilioni ya watu wengi, vilevile huwatilia umuhimu marafiki wa uislamu waliokaribu na uislamu na wenye kupendezwa na baadhi ya mambo yake, na pia kinawatilia umuhimu maadui wa uislamu na wenye kuuchukia na kukaa nao mbali, na wale ambao huenda ikawa kutokuujua uislamu ikawa ni moja ya sababu ya msingi ya kuufanyia uadui na kuuchukia uislamu.
Na miongoni mwa wanaopewa kipaumbele na kitabu hiki kwa nafasi ya juu kabisa ni wale waislamu ambao wanapenda kuifafanua dini ya uislamu kwa watu, Basi kitabu hiki kinawafupishia jitihada na kuwafanyia wepesi na kinawapunguzia kazi pia.
Na kwa hakika unaweza kukuta ewe msomaji mwenye akili timamu-kama ulikuwa huna fikra ya uislamu huko nyuma- kuwa wewe unahitajia kutilia umuhimu wa hali ya juu na kusoma kwa umakini ili ujue maana iliyogubikwa na kitabu hiki, na wala usione dhiki kwa hilo kwani kuna tovuti nyingi za kiislamu zinazojibu maswali yako.